PICHA & KAULI YA NAY WA MITEGO BAADA YA KUACHIWA HURU
Mwanamuziki Nay wa Mitego ameachiwa huru kutoka katika Kituo cha Polisi
cha Kati Dar es Salaam ikiwa ni saa chache tangu Rais Dkt Magufuli
aliporuhusu kuchezwa redioni kwa wimbo wake uliokuwa umefungiwa na
BASATA.
Agizo hilo la Rais Magufuli limetolewa leo na Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Mwakyembe alipokuwa akizungumza na
waandishi habari mkoani Dodoma.
Waziri Mwakyembe alisema kuwa Rais Magufuli amesema wimbo huo ni mzuri,
na kumshauri Nay wa Mitego aongezee mambo mengine kama kuwataja watu
ambao wanakwepa kodi, watumiaji wa dawa za kulevya.
Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia jana ambapo alipelekwa katika
Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi
cha Kati jijini Dar es Salaam.
Baada ya kutoka, Nay wa Mitego amezungumza na waandishi wa habari na
kuwashukuru wale wote waliojitokeza na kumsaidia kwa namna yoyote ile.
Amewashukuru Watanzania wote lakini pia wasanii waliokwenda kumuona na
kumtumia jumbe za kumpa moyo, lakini pia mawakili wake waliopambana kwa
muda wote kuhakikisha kuwa haki yake inakuwepo na kulindwa.
"Asante kwa wote walioamka na kuwa upande wangu, upande wa haki,
walioamini kile ambacho nimekifanya nawashukuru sana". Amesema Nay wa
Mitego