Singita Grumeti Fund Wakabidhi Mradi wa Maji kijiji cha Iharara Serengeti Mkoani Mara.

 Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akikata utepe kama ishara ya kupokea mradi wa maji Mtiririko katika kijiji cha Iharara uliojengwa na Kampuni ya Singita Grumeti Fund kwa ushirikiano na Shule ya Sekondari ya Issenye na wananchi,kulia kwake ni Mkurugenzi wa Singita Grumeti Fund Stephen Cuniliffe.

 Picha ya pamoja baada yauzinduzi,kutoka kushoto ni afisa maendeleo ya jamii kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Molel,Mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Iharara Goroban Mahega,Dc Nurdin Babu ,afisa mtendaji wa kijiji John Wangembe,afisa mtendaji wa kata ya Nagusi Molel na  Mkurugenzi wa Singita Grumeti Fund Stephen


 Picha ya pamoja na wanafunzi wa Issenye sekondari katika eneo la matenki yanayopokea maji kutoka kwenye tenki kubwa kwa ajili ya matumizi ya shule.

 Mkuu wa wilaya akifungulia bomba kuhakikisha maji yanayotoka kwenye chanzo cha maji mtiririko kwa kutumia umeme wa mionzi ya jua.



 Afisa maendeleo ya jamii kampuni ya Singita Grumeti Fund Frida Mollel akitoa taarifa ya mradi.


                                           Pandeni miti kote huko Dk akitoa maelekezo






Makamu Mkuu wa shule ya Issenye Ezekiel Onderi akitoa maelezo jinsi mradi utakavyowapunguzia wanafunzi na walimu umbali wa kutafuta maji.

 Mwenyekiti wa serikali ya Kijiji cha Iharara Goroban Mahega akishukuru kwa kupata mradi wa maji safi na salama kwenye kijiji chake na taasisi ya shule.

 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Serengeti William Makunja akihimiza wananchi kushikamana na wawekezaji ili waweze kutatua changamoto zinazowakabili.


                                Dc anasaini makabidhiano ya mradi huo wa Maji kulia ni Mkuu wa idara ya Maendeleo ya Jamii  Singita Grumeti Fund Frida Mollel



                              Makabidhiano yamekamilika wanapongezana.

  Lango la kuingia katika chanzo kikuu cha maji eneo la mashambani linafunguliwa rasmi

Tunzeni miundo mbinu atakayehujumu atashughulikiwa kwa mjibu wa sheria.

Mkuu wa wilaya Serengeti  akitwisha Ndoo ya Maji mmoja wa wanachi



 Singita Grumeti Fund katika kutekeleza Miradi  ya maendeleo kwenye vijiji 21 vinavyozunguka pori tengefu la Ikorongo/Grumeti limefanikiwa kwa kuwafikia wanakijiji cha Iharara kwa kuwapatia Mradi wa Maji  mbali na Miradi Mingine.

 

Akisoma Taarifa Mbele ya mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu  Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Singita Grumeti fund Frida Mollel amesema kuwa mwaka 2016 -2017 Singitra Grumeti Fund imefadhili mradi wa maji  Mtiririko katika kijiji cha Iharara wenye gharama ya shilingi 96,997,275 kwa kutoa asilimia( 82.15%).

 

“Mradi huu umefanywa na Singita kwa kushirikiana na Wanakijiji na wanakijiji wamechangia asilimia2.85 na shule ya Sekondari Issenye imechangia Asilimia  15 ya fedha zote za mradi” alisema Frida.

 

Hata hivyo Frida ameongeza kuwa mradi huo baada ya kukamiliki una miundombinu ya birika la mifugo vituo 2 vya kutolea maji na Tanki kubwa la ujazo wa lita 50,000 kwa ajili ya kukusanya maji  na Matanki ya kuifadhi maji yenye ujazo wa lita 20,000 pamoja na pampu ya mfumo wa jua unaopeleka maji katika shule ya sekondari issenye.

 

Baada kukamilika kwa mradi huo zaidi ya wanakijiji 1,500 Walimu na wanafunzi 500 wananufaika huku mifugo 2000 na yenyewe kunufaika na Mradi huo wa Maji.

 

Pia Singita  wametekeleza Miradi mingine ya Maji katika wilaya ya Serengeti na Bunda kama ifuatavyo,  Visima  virefu vya pump 38 sawa na shilingi 722,000,000, Matanki ya kuvunia maji  ya mvua  ya ujazo wa lita 5,000 zipo 17 kwa ghalama ya shilingi 323,000,000 , Marambo matatu ya mifugo na Visima vya asili vilivyoboreshwa 10 kwa gharama ya shilingi 483,614,248. 

Lengo ni kuhakikisha wanachi wote wanaondokana na changamoto ya uhaba wa maji safi na salama.

 

  Kwa upande wake Mkurugenzi wa Singita Grumeti Fund Stephen Cunliffe amewataka wanakijiji na uongozi wa shule kulinda  miundombinu ya maji ili itumike na kizazi kijacho huku mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu akisisitiza suala zima la upandaji miti katika vyanzo vya maji.

 

Nao baadhi ya Wananchi wakiwemo Wanafunzi wameshukuru uwepo wa Mradi huo na kuzidi kuomba Singiti kuendeleza kutekeleza Miradi Mbali katika sekta ya  Elimu na Afya.

Powered by Blogger.