TIMU YA TAIFA YA RIADHA YAKABIDHIWA BENDERA KUELEKEA UGANDA.
Rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania
(RT) Anthony Mtaka akikabidhi Bendera kwa manahodha wa timu ya taifa ya
riadha kwa upande wa wanaume,Fabian Joseph (kushoto) na Magdalena Shauri
(kulia)Wengine ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Hifadhi za Taifa
(TANAPA) Nyamakumbati Mafuru (mwenye miwani) ,Meneja Mawasiliano wa
TANAPA,Pascal Shelutete na kushoto ni Meneja wa timu ya taifa ya riadha
Meta Petro.
Raisi wa Shirikisho la Riadha Tanzania
,Anthony Mtaka akizungumza na wanariadha 28 wanaoelekea nchini Uganda
kwa ajili ya Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika wakati wa hafla fupi
ya kuwaaga iliyofanyika katika ofisi za Makao Makuu ya TANAPA jijini
Arusha.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) Nyamakumbati Mafuru akitoa neno kwa wanariadha
hao,Shirika la Hifadhi za Taifa ndilo limedhamini wanariadha hao ambao
idadi yao katika ushiriki wa mbio hizo imevunja rekodi ya tangu mwaka
1991.
Baadhi ya wanariadha watakao iwakilisha nchi katika mashindano hayo yatakayofanyika jumapili hii.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Whilleam Gidabuday akizungumza wakati wa hafala hiyo.
Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi
za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akizungumza wakati wa hafla ya
kuwaaga wanariadha wa timu ya taifa iliyoandaliwa na shirika hilo jijini
Arusha.
Kikosi cha wanariadha 28 na viongozi 12
kitakachopeperusha Bendera ya Taifa nchini Uganda katika Mashindano ya
Dunia ya Mbio za Nyika yatakayofanyika Jumapili hii katika mji wa
Entebe.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.