MUWSA WATUMIA MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI KUOTESHA MITI KATIKA VYANZO VYAKE VYA MAJI.
Baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka ya
Majisafi na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakishusha miti
tayari kwa ajili ya kuotesha kando ya vyanz vya maji vinavyosimamiwa na
mamlaka hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi
na Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) John Ndetiko akiwa amebeba
mti tayari kwa ajili ya kuotesha kando ya chanzo cha maji cha Shiri
kilichopo wilayani Hai.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi wakisaidia katika zoezi la ubebabji miti kwa ajili ya kuotesha.
Wafanyakazi wa MUWSA wakiwa wamebeba mit kwa ajili ya kuotesha katika chanzo cha maji cha Shiri.
Kaimu Mkurugenzi wa MUWSA,John Ndetiko akiotesha mti katika eneo la chanzo cha maji cha Shiri.
Baadhi ya wafanyakazi wa MUWSA wakiotesha miti katika chanzo hicho.
Hii ni sehemu ya mitiiliyooteshwa Mwaka
jana katika eneo hilo zoezi lililooongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro
Saidi Mecky Sadicki.
Huu ndio mti uliooteshwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Saidi Mecky Sadicki katika eneo hilo.
Chanzo cha maji cha Shiri kilichopo
wilayani Hai kinachoimamiwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira
mjini Moshi.(MUWSA.)
Wafanyakazi wa Mamlaka ya Majisafi na
Usafi wa Mazingira mjini Moshi (MUWSA) wakiwa katika picha ya pamoja
mara baada ya kuotesha miti katika chanzo hicho.
Chanzo kipya cha maji cha Mkashilingi kilichopo jirani na chanzo cha chemichei cha Shiri.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.