|
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina
Madete(katika) akitembelea maeneo ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT)
alipokuwa mgeni rasmi katika halfa ya kuzindua Kozi mpya za Masomo International
Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo
Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya
usafirishaji nchn.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa NIT, Profesa
Blasius Nyichomba na Mhandisi Dkt.
Prosper Mgaya.
|
|
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina
Madete akizungumza na wageni waalikwa katika halfa ya uzinduzi wa Kozi mpya za
Masomo ya International Computer Driving
Licence (ICDL) na Geographic Information
System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la
kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi
wa NIT, Profesa Blasius Nyichomba.
|
|
Mwenyekiti wa Baraza
la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Blasius Nyichomba akifafanua
jambo wakati wa halfa ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence
(ICDL) na Geographic Information System
(GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la
kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete.
|
|
Kaimu Mkuu wa Chuo
cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya akifafanua jambo
wakati wa halfa ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) leo
Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya
usafirishaji nchini.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi
wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Blasius Nyichomba.
|
|
Mkuu wa Idara ya
Tehama kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) Leticia Edward Mihayo
akielezea jambo wakati wa halfa ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence
(ICDL) na Geographic Information System
(GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la
kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete na jamboMwenyekiti
wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Blasius
Nyichomba.
|
|
Mwakilishi Mkazi wa Shirikala la Kimataifa la ICDL
Afrika, Edwin Masanta akizungumza jambo wakati wa halfa ya uzinduzi wa Kozi
mpya za Masomo ya International Computer
Driving Licence (ICDL) na Geographic Information
System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la
kuboresha sekta ya usafirishaji nchini. |
|
Mratibu wa Mafunzo ya
Mfumo wa Taarifa za Kijiografia (GIS) Bw. Isaya.J akizungumza jambo wakati wa halfa
ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International
Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic
Information System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa
lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini. Kutoka kulia ni Kaimu Mkuu wa
Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya, Naibu Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi
Angelina Madete na Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT), Profesa Blasius Nyichomba.
|
|
Baadhi ya wafanyakazi
wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Kozi
mpya za Masomo ya International Computer
Driving Licence (ICDL) na Geographic Information
System (GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la
kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.
|
|
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina
Madete(kushoto) akimsikiliza Mkufunzi wa Uhandisi wa Ndege Mhandisi Abubakar
Noor alipotembelea chumba cha mafunzo ya urubani katika Chuo cha Taifa cha
Usafirishaji (NIT) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Kozi mpya za Masomo ya International Computer Driving Licence
(ICDL) na Geographic Information System
(GIS) leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi
wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Profesa Blasius Nyichomba na Kaimu
Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT) Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya.
|
|
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina
Madete akiwakabidhi vyeti vya kutambulika kuwa wakufunzi wa Kozi mpya za Masomo
ya International Computer Driving Licence
(ICDL) na Geographic Information System
kutoka Idara ya Tehama (CCT) NIT wakati wa hafla ya uzinduzi wa kozi hizo leo
Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa Cha Usafirishaji
(NIT), Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya.
|
|
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina
Madete akipokea Cheti kutoka kwa Mwakilishi wa ICDL Afrika, Bw. Edwin Msanta
(kulia) kwa niaba ya NIT ikiwa ni ithibati ya uanzishwaji wa Kozi mpya za
Masomo ya International Computer Driving
Licence (ICDL) na Geographic Information
System leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa
Cha Usafirishaji (NIT), Mhandisi Dkt. Prosper Mgaya.
|
|
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina
Madete akikata utepe ikiwa ni ishara wa uzinduzi wa jengo la maabara ya
Kopmpyuta kwa ajili ya mafunzo ya Kozi mpya za International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) zitakazokuwa
zikifundishwa katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Jijini Dar es
Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.
Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa NIT, Profesa Blasius Nyichomba.
|
|
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina
Madete akiangalia Kopmyuta mara baada ya kufungua rasmi jengo la maabara ya
Kopmpyuta kwa ajili ya mafunzo ya Kozi mpya za International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic Information System (GIS) zitakazokuwa
zikifundishwa katika Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) leo Jijini Dar es
Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya usafirishaji nchini.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa NIT, Profesa Blasius Nyichomba.
|
|
Naibu Katibu Mkuu wa
Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Mawasiliano) Mhandisi Angelina
Madete (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa
Idara ya Tehama kutoka Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) mara baada ya
kuzindua Kozi mpya za International
Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic
Information System (GIS) zitakazokuwa zikifundishwa katika Chuo hicho leo
Jijini Dar es Salaam. Kozi hizo zimeanzishwa kwa lengo la kuboresha sekta ya
usafirishaji nchini.
Picha
zote na: Frank Shija
|
Na:
Frank Mvungi
Serikali
kupitia Chuo cha Usafirishaji (NIT) imedhamiria kutumia Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) kutekeleza azma ya kuifanya Tanzania kuwa nchi ya uchumi
wa kati.
Ili
kufanikisha azma hiyo Serikali imepanga kutumia chuo hicho kuwa kitovu cha
kuzalisha wataalamu watakaozalisha ajira na kuchangia kwenye ujenzi wa uchumi
wa viwanda.
Kauli
hiyo imetolewa leo Jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya ujenzi
Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano) Mhandisi Angelina Madete wakati
akizindua kozi za International Computer Driving Licence (ICDL) na Geographic
Information System (GIS).
“Nimefarijika
sana kusikia kwamba mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
yajulikanayo kama International License (ICDL) yanayotolewa katika nchi
zipatazo 100 kote duniani sasa yatakayopatikana katika Chuo chetu cha Usafirishaji (NIT) kwa
gharama nafuu” alisisitiza Madete.
Akifafanua
Madete amesema kuwa kwa sasa TEHAMA ikitumika ipasavyo itawanufaisha wananchi
kiuchumi na kijamii kupitia Sera Mpya ya Taifa ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
ya mwaka 2016.
Pia
Madete alibainisha kuwa hatua ya kukuza TEHAMA katika Chuo cha Usafirishaji
itaongeza ufanisi katika utekelezaji wa juhudi nyingine za Serikali zikiwemo
utekelezaji wa mfumo wa anuani za makazi na postikodi unaowezesha utambuzi wa
makazi kwa kila mwananchi.
Faida
nyingine ni kuiwezesha Serikali kutoa huduma kwa wananchi wake kwa urahisi na
ufanisi na pia kusaidia katika ukusanyaji wa kodi.
Mafunzo
yatakayotolewa na Chuo cha Usafirishaji ni hatua muhimu kwa Serikali ya Awamu
ya Tano kwa kuwa yanawezesha Taifa kuwa na wataalamu wanaozalisha ajira na
ujuzi unaoendana na mahitaji ya soko kwa sasa.
Kaimu
Mkuu wa Chuo hicho Mhandisi Dkt. Prosper
Mgaya akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Chuo hicho alisema kuwa chuo hicho
kimejipanga kujenga maabara 10 kwa ajili ya mafunzo (TEHAMA).
Naye
mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Prof.
Blasius Nyichomba alisema kuwa dhamira ya chuo hicho ni kuwa kitovu cha
mafanikio ndio maana kimeweza kuwa na kozi zinazotambulika kimataifa.
Aliongeza
kuwa kozi zinazotolewa na chuo hicho zinalenga kutatua changamoto katika sekta
ya Usafirishaji, Masoko,TEHAMA na nyingine kulingana na mahitaji ya wakati.