Serikali Yasaini Mkataba Wa Kuwakopesha Watumishi Wa Umma Mitungi Ya Gesi Na Vifaa Vyake
Serikali imesaini mkataba na Kampuni ya Gesi ya Mihan Gas wa kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vyake kwa watumishi wa umma.
Hatua
hiyo inakuja ikiwa ni juhudi za Serikali za kutaka kupunguza matumizi
ya mkaa pamoja na kuni kwa lengo la kutaka kuhifadhi misitu ambayo
imekuwa ikitumika kama nishati.
Mkataba
huo ulisainiwa jana Jijini Dodoma na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma
za Misitu Tanzania (TFS),Profesa Dos Santos Silayo na Mkurugenzi
Mtendaji wa Mihan Gas,Hamisi Ramadhan na huku Katibu Mkuu wa Wizara ya
Maliasili na Utalii,Mej. Gen. Gaudence Milanzi akishuhudia tukio hilo.
Mbali
na kusaini mkataba huo, TFS na Kampuni ya Mihan Gas zilizindua kampeni
ya kukopesha mitungi ya gesi na vifaa vya vyake kwa Watumishi wa Umma.
Awali,
Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Milanzi aliwahimiza
watumishi kuchangamkia fursa hiyo ya kukopa mitungi na vifaa hivyo
kwani itasaidia katika kuokoa misitu.
“Hili
ni tukio kubwa hasa kwa wale ambao ni watunzaji wa mazingira katika
kuwezesha jamii kuanza kutumia nishati mbadala.’’ Alisema
Naye,
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Misitu zaTanzania (TFS),Profesa Dos Santos
Silayo,alisema upatikanaji wa huduma hiyo ni jitihada za kuhakikisha
matumizi ya mkaa yanapungua
Aliongeza kuwa nishati mbadala ndo njia pekee itakayosaidia jamii kuachana na matumizi ya mkaa na kuni.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo,Hamisi Ramadhani
aliishukuru Serikali kwa kuikubalia kampuni hiyo kusambaza gesi kwa
watumishi.
Akizungumzia
namna watumishi watakavyonufaika na mpango huo, Mkurugenzi Mtendaji ,
Ramadhani alisema kampuni imetenga fungu ambalo litarahisisha ukopeshaji
wa vifaa hivyo na kila Mtumishi atapewa nafasi ya kuweza kulipia mwezi
mmoja mara baada ya kuanza kuitumia gesi.