Video: Mbunge John Heche na Matiko waripoti Polisi watakiwa kuripoti tena Agosti 14 Mwaka huu, Waongea na Vyombo vya Habari.

Kutoka
kushoto wa pili ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini CHADEMA John
Heche  katikati ni Makamu Mwenyekiti Kanda ya Serengeti CHADEMA ambaye
pia ni Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti wa Wilaya ya
Itilima CHADEMA Gimbi Masaba  anayefuata ni Mbunge Jimbo la Tarime Mjini
Esther Matiko wakitoka kituo cha Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya kwa
ajili ya kuripoti kutokana na Tuhuma zinazowakabili ikiwemo ya
Uchochezi na kuhamamsisha kilimo cha Bhangi.




Kushoto
ni Makamu Mwenyekiti Kanda ya Serengeti CHADEMA ambaye pia ni Mbunge
wa Viti maalum Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti wa Wilaya ya Itilima CHADEMA
Gimbi Masaba  akiteta jambo na Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini  Esther
Matiko katika ofisi za Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya hii leo.
Mbunge
wa Jimbo la Tarime Vijijini CHADEMA John Heche ambaye anatuhumiwa kwa
Makosa Mawili likiwemo la Kuruka Dhamana na Kuchochea wananchi  akiwa
Bungeni kuvamia Mgodi wa Uchimbaji wa Dhahabu ACACIA Uliopo Nyamongo
Wilayani Tarime na Esther Matiko mbunge Jimbo la Tarime Mjini
anayetuhumiwa kwa kosa la kuchochea wanachi kulima zao la Bhangi
wakifafanua jambo.
Kutoka
kushoto ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime ambaye pia ni
Diwani wa kata ya Nyamwaga CHADEMA Moses Misiwa akifuatia Mbunge wa
Jimbo la Tarime Vijijini John Heche ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA
Kanda ya Serengeti akifuatia Makamu wake ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum
CHADEMA  Mkoa wa Simiyu na Mwenyekiti wa Wilaya CHADEMA Wilaya ya
Itilima Mwisho kulia ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko
kipindi wakiongea na Vyombo vya habari katika Ofisi za chama hicho baada
ya kutoka kuripoti Polisi.
Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini John Heche akiongea na Vyombo vya habari
Mbunge Heche akieleza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inavyolinda wabunge

TAZAMA VIDEO WABUNGE WALICHOSEMA BAADA YA KUTOKA KURIPOTI POLISI AMBAPO PIA WANAPASWA KURIPOTI  TENA AGOST 14 MWAKA HUU.

Powered by Blogger.