RC Makonda Apokea Vifaa Vyenye Thamani Milion 400 Kwaajili Ya Ujenzi Wa Ofisi Za Walimu
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhiwa vifaa vya
ujenzi vyenye thamani ya shilingi Million 400 kutoka kiwanda cha MMI
Steel ltd kwaajili ya kampeni ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Dar es
salaam.
Vifaa
alivyokabidhiwa ni Mabati 15,000 yenye thamani ya shilingi Million 360,
Nondo Tani 22 zenye thamani ya million 40 ambapo kiwanda hicho
kimemuahidi tena kumpatia RC Makonda vifaa vingine ikiwemo Rangi, Nondo
na Mabati.
Akipokea
vifaa hivyo RC Makonda ameshukuru kiwanda cha MMI Steel chini ya
mkurugenzi wake Subhash Patel kwa kuwa mdau mkubwa wa kampeni ya ujenzi
wa ofisi za walimu na kuwasihi wadau na wananchi kujitokeza kuchangia
kampeni hiyo ili kutoa heshima kwa walimu.
Aidha
RC Makonda amesema kampeni ya ujezi wa ofisi za walimu inaendelea
vizuri ambapo hivi karibuni atapokea kontena nyingine 16 za furniture
kutoka Marekani, Kontena 10 za Vitabu kwaajili ya Maktaba ya jamii
kutoka Marekani, Kontena 10 za vifaa tiba kutoka uingereza na kontena 10
za Maziwa kutoka China kwaajili ya watoto waliojitokeza wakati wa Zoezi
la kutafuta haki ya watoto waliotelekeza Kama sehemu ya msaada.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha MMI Steel Ltd Bwana Subhash Patel
amesema wameamua kutoa vifaa hivyo kama sehemu ya kutambua umuhimu wa
elimu na kuunga mkono jitiada za RC Makonda katika uboreahaji wa elimu
kupitia mazingira bora ya walimu kufanya kazi.