Wakili: Afya ya Rugemarila, Seth zinatia mashaka
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu
imeelezwa kuwa afya ya mmiliki wa IPTL, Harbinder Singh Sethi na
mfanyabiashara James Rugemarila zinaendelea kuwa za mashaka.
Hayo
yameelezwa leo mapema na Wakili wa utetezi, Respicius Didas baada ya
Mwendesha Mashtaka kutoka Taasisi ya kizuia na kupambana na Rushwa
(Takukuru) Leornad Swai kudai kuwa upelelezi katika kesi hiyo bado
haujakamilika.
Mbele
ya Hakimu Mkazi Mkuu Huruma Shahidi Wakili Swai ameomba kesi hiyo
iahirishwe na kwamba walienda Magereza kuchukua maelezo ya Seth lakini
ilishindika kwa sababu afya yake haikuwa nzuri.
Kutokana
na taarifa hiyo, Wakili Didas alidai kuwa wakati afya za washtakiwa
zikiendelea kuwa za mashaka wanauomba upande wa mashtaka ukamilishe
upelelezi.
Amesema
ni vema kila kesi hii inapoahirishwa baada ya siku 14 kuwe na kitu
kipya kuhusu hatua zilizochukuliwa, lakini inavyoonekana upande wa
mashtaka unachukulia kawaida kuahirishwa kwa kesi hiyo.
"Upande wa mashtaka unacheza na mamlaka, utambue hali za washtakiwa ni mbaya, hivyo ukamilishe upelelezi" amesema Wakili Didas.
Swai
alidai, Serikali inajitahidi kuangalia afya za washtakiwa kwani hata
mara ya mwisho Serikali ilizungumzia afya ya Seth ambaye alidai anataka
madaktari wake wawepo wakati akifanyiwa upasuaji.
Kuhusu
upelelezi, Swai amedai ni kweli unachukua muda mrefu ila upo katika
hatua za mwisho na kitu kinachochelewesha ni upelelezi mwingine kuwa nje
ya nchi (Malysia)
Mshtakiwa
Rugemarila aliieleza Mahakama kuwa hajawahi kupelekwa Hospital ya Taifa
Muhimbili kwa ajili ya matibabu, pia anahisi ana Cancer kwa sababu ya
uvimbe alionao, pia Swai amesema daktari wake alisema hana cancer,
"anabahati amefiwa angekuja Mahakamani kusema kwamba nina cancer,"
Hakimu
Shaidi amesema Mahakama hiyo haina mamlaka ya kutoa amri wakatibiwe nje
ya nchi na alishatoa amri kwamba watibiwe Muhimbili na kama inahitajika
wakatibiwe nje ya nchi serikali ndio itasimamia.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 16, mwaka huu
Kwa
pamoja washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka 12 ya uhujumu uchumi,
utakatisha fedha na kuisababisha Serikali hasara ya USD 22, 198,544.60
na Sh.Bil 309.