Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro amekabidhi hundi za mikopo
shilingi milioni 25 kwa vikundi vitatu vya vijana na kimoja cha wanawake
zilizotolewa na halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Fedha hizo zinatokana na asilimia 10 ya makusanyo kutoka katika vyanzo
vya mapato ndani ya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga kwa kipindi cha
kuanzia Mwezi Julai 2o17 hadi Disemba 2017.
Vikundi vilivyokabidhiwa hundi ni kikundi cha Wanawake na Maendeleo
kilichopo katika kijiji cha Ishololo kata ya Usule na vikundi vya vijana
vya Umoja wa bodaboda, Jikwamue, Shukrani Group vilivyopo katika kijiji
cha Didia kata ya Didia katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Akikabidhi hundi hizo kwa wawakilishi wa vikundi hivyo leo Ijumaa
Februari katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo,Matiro aliwataka
walionufaika na mikopo hiyo watumie pesa walizopata kwa malengo
yaliyokusudiwa.
“Kila mtu aliyepata pesa akafanye kile alichokusudia kufanya, serikali
inajitahidi kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo ili mjikwamue
kiuchumi,naomba mfanye kazi kwa bidii ili kubadilisha maisha
yenu”,alieleza Matiro.DC