TLS Wamwagia Sifa Rais Magufuli
Makamu
Mwenyekiti wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Godwin Ngwilimi
amepongeza Rais John Magufuli kwa kutekeleza matarajio ya watanzania.
Ngwilimi
ametoa kauli hiyo leo Februari mosi jijini Dar es Salaam wakati wa
kilele cha Maadhimisho ya 22 ya siku ya Sheria na uzinduzi wa mwaka mpya
wa kimahakama.
Pia,
ameomba uwezeshaji wa rasilimali fedha katika muhimili wa mahakama ili
kushughulikia changamoto zinazoikabili. "Kama chama cha mawakili,
tunakuunga mkono na tunaahidi kutoa ushirikiano kwa mahakama pale
inapostahili."
Ametoa
wito akisema, watumishi wa mahakama, majaji, wasajili, watendaji ,
makarani na watumishi wengine, mawakili, wanasheria popote walipo
wanatakiwa kutambua mwelekeo wa nchi unabadilika kwa kasi, matarajio ya
wananchi , kuondokana na utamaduni wa kuendelea kufanya kazi kimazoea,
kutumia fursa zilizopo ikiwamo Tehama ili kuboresha huduma kwa wananchi.
Pia
kuendelea kusimamia maadili ya kitaaluma na uadilifu , hata Mungu
anapenda uadilifu na imeandikwa katika vitabu vitakatifu, kulinda na
kuhifadhi misingi ya kitaaluma na kujifunza kwa kufuata makosa
yaliyotokea hapo nyuma
Ngwilimi
ametoa wito akisema: " Kama sehemu ya watanzania, tusitumie mahakama
vibaya, kusumbua wengine, kuonea wengine, kama sehemu ya majaribio, siyo
maabara , kama jumba la kamari.