MWALIMU AFARIKI KWA KUKOSA PESA YA KUNUNUA DAWA YA MAFUA
Mwanamke mmoja anayejulikana kwa jina la
Heather Holland, 38, ambaye alikuwa mwalimu amefariki dunia baada ya
kushindwa kununua dawa ya mafua kutokana na gharama yake kuwa kubwa
nchini Marekani.
Kwa mujibu wa mume wa marehemu Frank
Holland, mkewe alipokwenda hospitali alikuta dawa hizo za mafua ni Dola
za Marekani 116 ambayo ni sawa na Tshs 278, 000 hivyo akaamua kuacha
kununua jambo lililosababisha kifo chake.
Frank amesema alikwenda kununua dawa
hizo siku moja kabla ya kifo cha mkewe ili aanze kuzitumia lakini
alikuwa amekwisha chelewa.
Heather ambaye alikuwa mwalimu wa Ikard
Elementary School huko Weatherford, Texas ameacha mume na watoto wawili,
wa kike mwenye miaka 10 na mwingine wa kiume mwenye miaka 7.
