Mtanzania ahukumiwa kunyongwa Uganda
Mahakama Kuu nchini Uganda imemuhukumu raia mmoja wa Tanzania kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya mauaji.
Mtanzania
huyo aliyetambulika kwa jina la Matule Chresporeto Coleheri mkazi wa
Bukoba anadaiwa kumuua mfanyakazi mwenzake katika shamba moja lililoko
eneo la Wakyuto wilayani Nakaseke.
Akisoma
hukumu hiyo, Jaji Steven Mubiru amesema baada ya kusikiliza ushahidi
uliotolewa na upande wa mashtaka, mahakama imejiridhisha kuwa Matule
ndiye alitenda kosa hilo.
Amesema
mashahidi watatu walioshuhudia tukio hilo wameiridhisha mahakama kuwa
Thomas Kamuhebwa aliuawa na mtuhumiwa huyo. Mwili wa Kamuhebwa ulikutwa
ukiwa umetupwa katika shimo moja na kufungwa katika begi. Mwili
uliokotwa karibu na makazi ya mshtakiwa.
Hata
hivyo, mbele ya mahakama hiyo Matule alijitetea kutohusika katika
mauaji hayo na kudai tuhuma hizo zilitengenezwa na watu waliotaka kuiba
magogo yake aliyoyaandaa kwa ajili ya kuzalisha mkaa.
Awali,
ilielezwa mahakamani hao kuwa Matule ni mhamiaji kutoka Tanzania
aliyekuwa akifanya kazi za vibarua na kwamba Februari 6, 2014 alimuua
Kamuhebwa kwa sababu zisizo julikana na kufukia mwili wake katika shimo.