KMC imeongeza idadi ya timu zinazotokea Dar es Salaam katika Ligi Kuu
Bara baada ya ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya JKT Mlale waliokuwa
vinara wa Kundi B la Ligi Daraja la Kwanza.
Ushindi huo unaifanya KMC kupanda Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza huku
shujaa wake akiwa ni kiungo mkongwe Abdulhalim Humud aliyefunga bao hilo
pekee.
Huenda furaha kuu itakuwa kwa kocha Fred Felix Minziro maarufu kama
Majeshi ambaye aliipandisha Singida United na sasa amejiunga na KMC na
kuipandisha pia.
JKT Mlale iliyokuwa nyumbani ilionekana ina nafasi kubwa zaidi ya
kupanda kwa kuwa ndiyo ilikuwa kinara ikiwa na pointi 25 sawa na KMC.
Lakini ushindi huo wa KMC umeifanya ifikishe pointi 28 na kupaa kileleni
ikifuatiwa na Coastal Union iliyoshinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Mawezi
mjini Morogoro. Coastal imemaliza ikiwa na pointi 26 wakati Mlale
wanabaki na 25.
KUNDI B
P W D L F A GD Pts
1. KMC 14 8 4 2 17 13 4 28
2. Coastal Union 14 7 5 2 18 9 9 26
3. JKT Mlale 14 7 4 3 13 7 6 25
4. Polisi Tanzania 14 6 6 2 18 12 6 24
5. Mbeya Kwanza 14 6 4 4 14 10 4 22
6. Mufindi 14 3 4 7 13 21-8 13