Whatsapp Yamponza Mbunge
Mbunge mmoja nchini Kenya ametakiwa kuomba radhi mara baada ya kutuma ujumbe wa kimapenzi kwenye group la Whatsapp la wabunge.
Anthony
Kiai alituma ujumbe wa kimapenzi kwenye group na kuwaomba wabunge
wenzake kutoutilia maanani kwani amekosea lakini wabunge wenzie katika
group hilo walimtaka kuomba radhi.
Aidha,
Admin wa group hilo, Bernad Chege, alimuomba mbunge huyo kuomba radhi,
na badala yake msaidizi wa Mbunge huyo ndio akaomba radhi kwa kitendo
hicho cha bosi wake kutuma ujumbe wa mapenzi katika group hilo
Ujumbe
huo ulioandikwa kwa lugha ya Gikuyu ambayo inaongelewa na Wakikuyu
nchini Kenya, ilikuwa ikitoa maelezo jinsi ya kumridhisha mwanamke
chumbani, huku baadhi ya wabunge wengine walionekana kumtetea wakisema
ngono sio dhambi.
Hata hivyo, Mbunge Kiai amekuwa mbunge wa jimbo la Mukurweini kufuatia ushindi alioupata kwenye uchaguzi wa Agosti 8, 2017