Mahakama Kuu Kenya yaondoa zuio la maandamano
Mahakama
Kuu nchini Kenya imeondoa kwa muda zuio la maandamano ya muungano wa
vyama vya upinzani nchini humo (NASA) katika miji ya Nairobi, Mombasa na
Kisumu lililowekwa na Serikali.
Zuio
hilo la kufanya maandamano katika miji hiyo ya kibiashara ilitolewa
wiki iliyopita na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Kenya, Fredi Matiangi ili
kuweza kuondokana na uharibifu ambao ungeweza kujitokeza, lakini zuio
hilo limeondolewa baada ofisa mtendaji mkuu wa Nasa, Norman Magaya
kufungua kesi mahakamani.
Aidha,
Jaji John Mativo ametoa zuio la kukamatwa kwa Magaya kutokana na
maandamano ya Nasa hadi kesi yake itakaposikilizwa na kutolewa hukumu.
Hata
hivyo, Katika kesi hiyo, Magaya amemfungulia kesi Inspekta Jenerali wa
Polisi, Joseph Boinnet, Mkurugenzi Mkuu wa Mashtaka, Keriako Tobiko na
Kaimu Waziri wa Mambo ya Ndani Fred Matiang’i kwa kuzuia maandamano
dhidi ya tume huru ya uchaguzi IEBC.