TAKUKURU YAMPA ONYO MBUNGE JOSHUA NASSARI
Taasisi
ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU imeita Waandishi leo Dar es
salaam na kutoa onyo kwa Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nassari
ambae alipeleka ushahidi wa rushwa kwa taasisi hiyo dhidi ya Mkuu wa
Wilaya Arumeru Alexander Mnyeti.
TAKUKURU
imesema “Ni kama Mh. Nassari na wenzie wanataka kulifanya hili swala
kama la kisiasa badala ya kuwa la kisheria, namuonya Mh. Nassari
ameshaleta taarifa yake kwetu, atuachie tufanye kwa mujibu wa sheria na
sio kutushinikiza kama kauli aliyoitoa jana….. ‘nitaendelea kutoa
series’ “
“Hii
Taasisi haishinikizwi na mtu yeyote na hapaswi hata mara moja
kutushinikiza…. natoa onyo jingine, endapo ataendelea na utaratibu huu
tutachukua hatua za kisheria dhidi yake”