Rais Magufuli: Sitaufuta Mwenye Wa Uhuru
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amesema hatafuta
Mwenge wa Uhuru katika kipindi chake cha uongozi kwasababu una faida
mbalimbali kwa taifa.
Hayo
ameyasema leo kwenye hotuba yake wakati akihitimisha mbio za Mwenge
mwaka huu sambamba na kuazimisha miaka 18 ya kifo cha Baba wa Taifa
kwenye sherehe zilizofanyika kwenye uwanja wa Amani Zanzibar.
Rais
Magufuli amesema kwenye awamu yake kamwe hatafuta mbio hizo kwani zina
saidia kufungua miradi mbalimbali ya maendeleo nchini pamoja na kumuenzi
Baba wa taifa Hayati Mwalimu Nyerere ambaye ndiye muasisi wa Mwenge wa
Uhuru.
“Nafahamu
kuna watu wanataka mbio za Mwenge zifutwe kwa kisingizio cha gharama
lakini wanasahau kuwa Mwenge huo unasaidia kuanzishwa na kukamilika kwa
Miradi ya maendeleo nchini. Nataka niwahakikishie kuwa kwenye uongozi
wangu na Dkt. Shein hatutafuta Mwenge wa Uhuru”, amesema Rais Magufuli.
Aidha
Rais Magufuli ameongeza kuwa mbio za Mwenge zimekuwa zikisaidia kubaini
madudu mbalimbali yanayofanyika kwenye Halmashauri nchini ikiwemo
Miradi hewa. Rais ameahidi kuipitia ripoti nzima ya mbio hizo na
kuyafanyia kazi mapendekezo yote yaliyoainishwa.