Hamisa. Sina Tatizo Na Zari wa Diamond
Mrembo Hamisa Mobetto amesema hana tatizo lolote na mpenzi wa Diamond, Zarina Hassan na anaamini siku moja watakuwa sawa.
Hamisa amesema hayo jana Ijumaa wakati wa sherehe maalum aliyoandaa kwa ajili ya mtoto wake Abdul Nassib.
Amesema licha ya kuwepo kwa maneno na hali ya kutoelewana kwa sasa anaamini utafika wakati watakuwa pamoja.
"Watoto
wameshatuunganisha, najua kwa sasa mambo na maneno ya watu ni mengi ila
ipo siku kwa sababu mtoto wangu ana ndugu na watoto wake basi tutakuwa
sawa tu.Maana inawezekana mtoto wangu akataka kuwatembelea ndugu zake au
wale wakamtaka ndugu yao kwa hiyo yote yanawekezekana," amesema