NEC Yasisitiza Amani Na Utulivu Uchaguzi Mdogo Wa Madiwani Katika Kata 43
NEC –DODOMA
Mkurugenzi
wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Bw. Kailima Ramadhan
amewaasa wadau wa uchaguzi kuhakikisha kuwa uchaguzi mdogo wa madiwani
utakaofanyika katika Kata 43, Novemba 26 unafanyika kwa amani na
utulivu.
Bw.
Kailima ameyasema hayo jana (Jumamosi) mjini Dodoma wakati wa
maandalizi ya mafunzo kwa Wasimamizi na Wasimamizi wasaidizi pamoja na
maafisa uchaguzi yanayotarajiwa kuanza leo (Jumapili) mjini hapa.
“Mlango
wa kuchukua fomu kwa ajili ya uteuzi utafunguliwa kuanzia tarehe 20 saa
moja na nusu asuhuhi mpaka 25 mwenzi huu, na fomu zinatakiwa kurejeshwa
na uteuzi utafanyika tarehe 26 mwenzi Oktoba saa kumi kamili jioni.
Nawasihi wadau wote wa uchaguzi tufanye uchaguzi wetu uwe wa amani na
utulivu, natumaini kama ambavyo nchi yetu ni kisiwa cha amani na kwa
jinsi tulivyojipanga (Tume) uchaguzi utakua wa amani na utulivu,”
alisema.
Bw.
Kailima alisema kuwa katika mchakato wa kuendea siku hiyo ya uchaguzi
NEC hairuhusu mikutano ya vyama vya siasa bali inaruhusu mikutano ya
kampeni.
“Tume
ya Taifa ya Uchaguzi hairuhusu mikutano ya vyama vya siasa, Tume
inaruhusu mikutano ya kampeni kwa muda wa siku 30 kuanzia tarehe 27
Oktoba mpaka tarehe 25 Novemba 2017, siku moja kabla ya uchaguzi.
Kampeni lazima ziendeshwe kwa utaratibu uliopangwa,” alisema Bw.
Kailima.
Akizungumzia
kuhusu maadili ya Uchaguzi, alisema kwa mujibu wa Kifungu Namba 124A
cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Tume, Serikali na vyama vya
siasa vyote vinapaswa kukubaliana na maadili ya uchaguzi ambayo
yalisainiwa na wadau wote tarehe Julai 27, 2015.
“Nitoe
wito kwa wadau wa uchaguzi kwamba pale ambapo patakua na ukiukwaji wa
maadili, malalamiko yapelekwe kwenye kamati husika saa 72 baada ya tukio
husika, kwa ngazi hii ya udiwani malalamiko yanatakiwa yapelekwe kwenye
kamati ya maadili ngazi ya Kata ambayo wajumbe wake ni vyama vyote vya
siasa vyenye wawakilishi walioteuliwa. Msimamizi msaidizi ngazi ya Kata
ndiyo mwenyekiti wa kamati,” alisema.
Bw.
Kailima aliongeza kusema kwamba endapo maamuzi hayataridhiwa wahusika
wanaruhusiwa kukata rufaa ngazi ya Jimbo ambapo msimamizi wa uchaguzi
atatoa maamuzi na endapo hayakuridhiwa jambo hilo litakua ni lalamiko la
uchaguzi baada ya uchaguzi kukamilika.
Mkurugenzi
huyo alisema kwamba mafunzo hayo yatahusisha washiriki 144 ambao ni
Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimizi wasaidizi na maafisa uchaguzi ngazi ya
Jimbo na Kata na yatafanyika kwa siku tatu kuanzia kesho Oktoba 15 hadi
17, 2017.
“Uchaguzi
huu mdogo utafanyika kwenye Kata 43 ambazo zipo kwenye mikoa 19,
Hamashauri 36 na Majimbo 37 kwa hiyo uchaguzi huu mdogo unafanyika
karibia maeneo ya nchi nzima,” alisema Kailima.