Waziri Mkuu: Tumuenzi Baba Wa Taifa Kwa Kuiga Maisha Yake
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewaomba Watanzania waendelee kumuenzi Hayati
Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere kwa kuiga maisha yake na utendaji
wake.
Ameyasema
hayo jana (Jumamosi, Oktoba 14, 2017) aliposhiriki ibada maalumu ya
kumuombea Mwl. Nyerere iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Minara
Miwili Zanzibar.
Ibada
hiyo ya kumbukumbu ya miaka 18 ya kifo cha Mwl. Nyerere ni sehemu ya
maadhimisho ya kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru uliozimwa jana katika
mkoa wa Mjini Magharibi visiwani Zanzibar.
Katika
Idaba hiyo Waziri Mkuu amewasisitiza wananchi kuhakikisha wanamuenzi
Mwl. Nyerere kwa kuendeleza mambo mema yote aliyoyafanya enzi za uhai
wake.
Awali,
Katibu wa Jimbo Katoliki Zanzibar Padri Cosmas Shayo ambaye aliongoza
ibada hiyo aliwaomba waamini wamuenzi Mwl. Nyerere kwa kudumisha umoja
na mshikamano wa Taifa.
“Hayati
Baba wa Taifa Mwl. Nyerere aliwapenda watu wote bila kujali Imani zao
wala itikadi zao. Alikuwa mzalendo na alitaka Watanzania waishi maisha
bora.”
Padri
Shayo aliongeza kuwa tunu za amani na umoja zilikuwa miongoni mwa
falsafa kuu ya Mwl. Nyerere, ambapo matokeo yake ni umoja na mshikamano
wa Taifa uliopo.
Ibada
hiyo ilihudhuriwa na Makamu wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
Balozi Seif Ally Idd, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,
Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Bi Jenista Mhagama, Mke wa Waziri Mkuu
Mama Mary Majaliwa.
Wengine
ni Waziri wa Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, Wanawake na Watoto Bi.
Mauldine Castico, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce
Ndalichako, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira Bw.
Anthony Mavunde, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Walemavu Bi. Stella
Alex Ikupa na mwakilishi wa familia ya Mwl. Bw. Makongoro Nyerere.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,