Mugabe amuandaa mkewe kumrithi
Rais
Robert Mugabe amekubali kugeuza kongamano la mwaka la Zanu PF
lililopangwa kufanyika Desemba kuwa mkutano mkuu wa congress
unaotarajiwa kutumika kumshusha Makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa na
kumpaisha mkewe Grace kuwania urais katika chama.
Kamisaa
wa Taifa wa Zanu PF Saviour Kasukuwere ndiye aliyependekeza suala la
mkutano wa congress alipokuwa anawasilisha ripoti yake kwenye kamati kuu
ya chama Jumatano lakini ilibainika kuwa kinara huyo wa kundi la G40
alikuwa amepata ushauri kutoka majimbo matatu tu.
"Mugabe
alisema utakuwa ukiukwaji wa taratibu hivyo akaagiza kamati ya
maandalizi kuhakikisha ushauri umepatikana kutoka majimbo yote. Kutakuwa
na vikao vya uratibu wa majimbo kutafakari suala hilo kuanzia mwishoni
mwa wiki hii.
"Mkutano
mkuu wa chama umepangwa ili kufanya mabadiliko ya katiba ili kuingiza
kifungu cha kuwa na makamu wa rais mwanamke au kuanzisha makamu wa tatu
wa rais,” mtu wa ndani alidokeza.
"Suala
la urais limekamilika lakini misuguano ya ndani kuhusu kuwania mamlaka
na umri wa Mugabe vimelazimisha kutafakari na Nyanja mbalimbali. Kumbuka
kuwa Grace anataka madaraka na amekuwa akiomba awe makamu wa rais
sambamba na Mnangagwa".
Msemaji wa Zanu PF, Simon Khaya Moyo amekataa kuzungumzia suala hilo.
Miezi
miwili iliyopita Mugabe aliwataka wajumbe wa Zanu PF kufikiria kuingiza
katika katiba nafasi ya makamu wa tatu wa rais. Hii ilikuwa baada ya
mkewe kumtaka kiongozi huyo mkongwe wa Zanu PF kumtangaza mrithi
anayempendelea katika mkutano mkuu wa wanawake.