Mbowe kuzungumzia afya ya Lissu, michango
Mwenyekiti
wa Chadema, Freeman Mbowe leo atazungumzia kinachoendea katika
hospitali ya Narobi nchini Kenya kuhusu afya ya Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha
chama hicho, Tumaini Makene, Mbowe atazungumzia hayo leo katika ofisi za
makao makuu ya chama hicho, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Pamoja na mambo mengine, Mbowe anatarajia kuzungumzia michango iliyokusanywa na matumizi yake.
“Kupitia
kwa Mwenyekiti Freeman Mbowe, chama kitatoa taarifa kuhusu maendeleo ya
Tundu Lissu, mrejesho wa michango na gharama za matibabu,” imeeleza
taarifa hiyo na kuongeza kuwa mkutano huo utafanyika majira ya saa tano
asubuhi.
Lissu
anaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya
kutokana na majeraha aliyoyapata kwa kushambuliwa na risasi akiwa ndani
ya gari, nyumbani kwake eneo la Area D mjini Dodoma.
Jana,
Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliwaambia watanzania
kupitia Instagram kuwa alimtembelea Lissu na kuliona tabasamu lake,
hivyo akawasihi waendelee kumuombea.