KIONGOZI WA UPINZANI RWANDA AMTAKA RAIS KAGAME AMWACHIE HURU
Kiongozi
wa upinzani nchini Rwanda, Diane Rwigara amemtaka Rais Paul Kagame
kumfutia mashtaka na kuwaachilia ndugu zake ambao wanashikili na jeshi
la polisi nchini humo.
Rwigara
amesema kuwa serikali imefanya jaribio la kuinyamazisha familia yake
pamoja na wafuasi wake tangu alipotangaza kuwania nafasi ya uraisi
katika uchaguzi uliofanyika mwezi Mei mwaka huu.
Aidha,
ndugu hao watatu ambao walikamatwa mwezi uliopita, wameshtakiwa kwa
makosa ya udanganyifu na uchochezi, tuhuma ambazo wameziita zenye mrengo
wa kisiasa.
Hata
hivyo,Rwigara alizuiliwa kuendelea na nia yake ya kuwania nafasi ya
urais wa Rwanda, Uchaguzi ambao Kagame alishinda kwa kishindo kwa karibu
asilimia tisini na tisa ya kura zote zilizopigwa