Lissu atoka ICU aona jua kwa mara ya kwanza tangu apigwe risasi .......Mbowe Asema Atasafirishwa Nje ya Nchi
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amesema kuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ametoka ICU na sasa anaweza kukaa.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo Jumanne, Mbowe amesema afya ya Lissu
inaimarika kwa kuwa alihitaji upasuaji mwingi sana kutokana na risasi
zilizoingia kwenye mwili wake.
“Amefanyiwa
upasuaji mkubwa mara 17 mpaka sasa. Ameongezewa damu nyingi kuliko mtu
yeyote miaka 20 iliyopita ametoka ICU wiki iliyopita,” amesema Mbowe.
Amesema Lissu hatumii oxygen tena wala mirija na kwamba anakula chakula anachokitaka.
“Juzi kwa mara ya kwanza alikaa, anatembea Wheel Chair na aliliona jua kwa mara ya kwanza,” amesema Mbowe.
“Tunawashukuru
madaktari wa Dodoma na Nairobi. Hospitali ya Nairobi imefikisha awamu
ya pili ya kutibu. Tunavyozungumza baada ya wiki moja kadri madaktari
watakavyoshauri atamaliza matibabu ya pili,”
“Ataanza
awamu ya tatu nje ya Nairobi yatakayokuwa ya muda mrefu. Kwa usalama
wake hatutataja wapi anakwenda. Siyo Tanzania na sio jirani. Hiyo ndio
hali halisi ya mgonjwa.”