Askari Aliyekuwa Akifanya Mapenzi na Mfungwa Ajinyonga
Askari
mmoja wa Chuo cha Mafunzo ya Wafungwa cha Losperfontein, nchini Afrika
Kusini amejinyonga hadi kufa mara baada ya kuzagaa kwa picha
zilizomwonyesha akimpiga busu mfungwa kusambazwa kwenye mitandao ya
kijamii .
Taarifa
iliyotolewa na Idara ya Magereza nchini humo imesema kuwa ilifahamishwa
kuhusu picha zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii na kwamba wakati
wanafanya uchunguzi wa tukio hilo, tayari ofisa huyo alikuwa
ameshajinyonga.
Aidha,
Kamishna wa Magereza wa Limpopo‚ Mandla Mkabela amesema katika taarifa
yao kwamba wameshtushwa sana na wamehuzunishwa mno na tukio hilo la
kujinyonga kwa Askari huyo.
“Tumetuma
timu ya mameneja waandamizi na wataalamu wa mpango wa ushauri kwa
wafanyakazi kwa ajili ya kutoa msaada wowote muhimu,” amesema Mkabela.
Hata
hivyo, Mkabela amelaani tukio la usambazaji wa picha zinazodaiwa kuwa
ni za ofisa huyo ambazo zimeweza kumsababishia kuchukua maamuzi ya
kujinyonga.