Jeshi la Polisi Lawapa Ujumbe ma Admin wa Whatsapp
Naibu
mkuu wa kitengo cha makosa ya mtandaoni, Joshua Mwangasa amewataka
viongozi wa makundi ya what’s App kutoa taarifa pindi uhalifu
unapofanyika katika makundi yao kwani kwa kiasi kikubwa makundi hayo
yamekuwa yakitumika kusambaza taarifa za uongo na uchochezi.
Ameeleza
kuwa kwa kufanya hivyo kwa kiasi kikubwa kutapunguza na kudhibiti
makosa mengi yanayofanywa mtandaoni na kutasaidia polisi kuchukua hatua
dhidi ya muhusika aliyefanya uhalifu huo.
Lengo
kubwa likiwi ni kukabiliana na ongezeko la vitendo vya uhalifu
mtandaoni huku makundi ya What’s App yakionekana kuwa kichocheo kikubwa.
“Usikubali
umeanzisha kundi kwa nia nyingine halafu mtu au watu wanaweka mambo
yasiyofaa, toa taarifa hatua zichukuliwe kinyume na hapo hata wewe
utahusika,” amesema Mwangasa.
Mwangasa
ametumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kuwahubiria waumini wao
juu ya matumizi sahihi ya mitandao ili kujiweka mbali na uhalifu.
“Ukosefu
wa maadili ndio unachangia haya yote haya, ndiyo sababu narudi kwenu
viongozi wa dini wasisitizeni waumini wenu watumie mitandao kwa
maendeleo,” amesema.
Kwa
upande wake Mkurugenzi wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema mamlaka
hiyo inaendelea kuchukua hatua kuimarisha ulinzi wa mawasiliano
mtandaoni.
Hayo
yamezungumwa jana katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya
Mawasiliano(TCRA) na kuwakutanisha viongozi wa dini wa Mkoa wa Dar es
Salaam.