Taarifa Kwa Umma Kuhusu Kuahirishwa Kwa Mnada Wa Tanzanite
Wizara
ya Madini inatoa taarifa kwa umma kuwa Mnada wa Madini ya Tanzanite
uliokuwa ufanyike katika mji mdogo wa Mererani Wilayani Simanjiro mkoani
Manyara kuanzia tarehe 12 hadi 15 Oktoba, 2017, umeahirishwa hadi hapo
utakapotangazwa tena.
Sababu
za kuahirishwa kwa mnada huo ni kuridhia maombi ya wadau wa mnada ambao
waliomba kupata muda zaidi wa maandalizi ili wapate fursa ya kushiriki
kwa wingi.
Aidha,
uongozi wa Wizara na Mkoa wa Manyara watapata muda zaidi wa kuandaa
mazingira salama na bora zaidi ya kufanyia mnada huo katika mji wa
Mererani.
Hivyo,
Wizara ya Madini inawaomba radhi wadau wote wa Sekta hii ndogo ya
madini ya vito hususan Tanzanite ambao wameathirika kwa namna moja au
nyingine kutokana na kuahirishwa ghafla kwa mnada huu.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini