Abiria wa Bodaboda na Mmliki Kuwajibishwa
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba amewataka abiria nchini
kuendelea kutii sheria za usalama barabarani vinginevyo itaundwa sheria
ambayo itawawajibisha.
Waziri
ameyasema hayo jana mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro kwenye uzinduzi wa
wiki ya Usalama Barabarani ambapo aligusia usafiri wa pikipiki maarufu
kama Bodaboda.
“Sheria
itabidi imtambue mmiliki kwenye kosa la dereva pikipiki kukosa kofia
ngumu (Helmet) ili wote wawajibishwe na hapo ndio wamiliki watakuwa
makini kuhakikisha vyombo vyao vina kofia ngumu mbili, ya dereva na
abiria”, alisema Mwigulu.
Aidha
waziri Mwigulu aliongeza kuwa kutokana na takwimu za ajali za Bodaboda
kuna haja ya kutumia taratibu ama sheria ambayo itamuwajibisha abiria
endapo hatavaa kofia ngumu hali ambayo itasaidia abiria kudai kofia
kabla ya kupanda Pikipiki.
Usafiri
wa Bodaboda umekuwa na msaada mkubwa maeneo ya mijini na vijijini
lakini umekuwa ukitajwa kama chanzo kikubwa cha ajali za barabarani
kutokana na madereva wake kutofuata sheria za barabarani.