Waziri Mkuu Atuma Ujumbe kwa 'Watu Wasiojulukana; Wanaofanya Matukio ya Kihalifu Nchini
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amesema serikali haitafumbia macho matukio ya
mashambulizi wanayofanyiwa watu mbalimbali wakiwepo viongozi na kuwataka
wabunge na wananchi kuendelea kuwa wavumilivu wakati jeshi la polisi
likiendelea kufanya uchunguzi.
Waziri
Majaliwa amesema hayo wakati akiahirisha vikao vya mkutano wa nane wa
bunge la 11, na kusema vyombo vya dola vinaendelea kufanya uchunguzi ili
kuwabaini watu wasiojulikana wanaojihusisha na vitendo hivyo ili
sheria iweze kuchukua mkondo wake.
"Serikali
haitofumbia macho matukio ya kihalifu yanayotokea nchini, vyombo vya
dola tayari vimeshaagizwa kuhakikisha wanawatafuta wanaohusika na
vitendo vya kihalifu na kukamatwa ili hatua za kisheria zichukuliwe
dhidi yao", amesema Waziri Majaliwa.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa Kamati ya kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje
Ulinzi na Usalama Mhe. Adad Rajabu ameliomba bunge kuongeza muda ili
kuweza kukamilisha kazi ya kufanya uchunguzi wa matukio ya kujeruhiwa,
kuvamiwa pamoja na kufuatiliwa kwa baadhi ya wabunge ili kuweza
kukamilisha kazi hiyo.
Aidha Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amehairisha vikao vya bunge leo hadi Septemba 7 mwaka huu ambapo litafunguliwa tena.