Jeshi la Polisi Lapiga Marufuku Maombi ya Kumuombea Tundu Lissu Yaliyotangazwa na CHADEMA
Kamishna
Kanda maalumu ya Dar es salaam, Lazaro Mambo Sasa amepiga marufuku
maandamano na maombi yanayotaka kufanywa na CHADEMA siku ya Jumapili
kumuombea Tundu Lissu kwenye uwanja wa TP Sinza Dar es Salaam na kusema
hiyo siyo sehemu ya maombezi.
Lazaro
Mambo Sasa amesema hayo leo wakati akifanya mahojiano na waandishi wa
habari na kusema kuwa hawezi kuruhusu mkusanyiko wa watu na kuwataka
watu ambao wanataka kumuombea Tundu Lissu kwenda kwenye nyumba za ibada
na kumuombea lakini si kufanya mkusanyiko huo ambao wao CHADEMA wanataka
kufanya.
"Hatutaruhusu
mkusanyiko wowote usio na kibali, yapo maeneo ambayo kimsingi
yanaendesha maombi hayo, yapo makanisa ipo misikiti na mahali pengine
ambako pengine ni rasmi kwa shughuli hiyo.
"Kupitia
kwenu nasema hakutakuwa na kusanyiko hilo, yapo maneno ambayo
yanaendelea kutolewa kupitia taarifa zao walizotoa ambayo maneno hayo
kimsingi kila anayesikiliza anajua nia yao ni nini.
"Na
sisi tukishaona kuna viashiria vya uvunjifu wa amani hatuwezi kuhurusu
mkusanyiko wa watu kwa hiyo mkusanyiko wa maombi hayo ni marufuku,
tunaruhusu mwenye uwezo hata wa kukesha kanisani aende kwani ni mahali
rasmi kwa maombi" alisisitiza Mambo Sasa
Aidha
Kamanda Mambo Sasa ametolea ufafanuzi juu ya wanachama wa CUF ambao
waliomba kufanya maandamano siku ya Jumapili Septemba 17, 2017 kwa ajili
ya kuwapokea baadhi ya wabunge saba wa chama hicho ambao wameapishwa
siku ya karibuni bungeni na kusema jambo hilo haliwezekani na yoyote
ambaye atakiuka maagizo hayo basi ataishia mikononi mwa polisi.
"Sambamba
na hilo naomba niseme kwa wale wanachama wa CUF ambao wameomba tarehe
17 kuwapokea wabunge wa CUF wanaotoka kuapishwa Dodoma walikuwa wameomba
kufanya maandamano waanzie Kimara kuelekea Buguruni tumeshatoa
maelekezo kuhusu hilo kuwa maandamano hayaruhusiwi na yoyote atakaye
jaribu kufanya maandamano ataishia mikononi mwa polisi" alisema Kamanda
Mambo Sasa
Baraza
la Vijana CHADEMA (BAVICHA) leo asubuhi lilitoa taarifa kwa umma kuwa
siku ya Jumapili litafanya maombezi ya kitaifa kwenye uwanja wa TP
uliopo Sinza Darajani kumuombea Mbuge Tundu Lissu ambaye alishambuliwa
na risasi na watu wasiojulikana ili aweze kupona kwa haraka na kurudi
kuendelea na shughuli zake, jambo ambalo limepigwa na jeshi la polisi.