Waziri Mkuu Atoa Msaada Wa Sh. Milioni 10
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa msaada wa sh. milioni 10 ili kumuwezesha Bw. Ernest Masenga kutatua changamoto zinazomkabili.
Bw.
Masenga alikuwa msanii wa muziki wa dansi ambaye sasa anasumbuliwa na
maradhi ya miguu. Pia makazi anayoishi si salama yanahitaji
kukarabatiwa.
Waziri Mkuu ametoa msaada huo jana (Jumatatu, Septemba 11, 2017) katika makazi ya Waziri Mkuu Oysterbay jijini Dar Es Salaam.
Ametoa
msaada huo baada ya kuguswa na hali ya maisha ya msanii huyo aliyemuona
kupitia kipindi maalumu kilichoonyeshwa na TBC Sempemba, 5, 2017.
Kipindi hicho kiliongozwa na Bw. Godfrey Nago.
“Nawaomba
Watanzania wenzangu tumsaidie mwezetu ili aweze kuishi vizuri kwa
sababu sanaa yake imesaidia katika kuelimisha na kuburudisha umma .”
Kwa
upande wake Bw. Nago ambaye amepokea msaada huo kwa niaba ya Bw.
Masenga amesema atahakikisha anasimamia vizuri fedha hizo ili zitumike
kama ilivyokusudiwa.
Pia
Bw. Nago amesema anamshukuru Waziri Mkuu kwa kuwaunga mkono na kutoa
msaada huo kwa sababu ameonesha kwamba Serikali inawajali wananchi wake
na TBC itaendelea kuwaomba wadau mbalimbali wajitokeze na kumsaidia
msanii huyo.
Naye
Mjomba wa msanii huyo Bw. Kanuti Mloka ambaye ameiwakilisha familia
amemshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo kwa kuwa familia imeshindwa
kumsaidia Bw. Masenga kutokana hali duni ya maisha waliyonayo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, SEPTEMBA 11, 2017.