Serikali Yawasilisha Bungeni Mkataba wa Kimataifa wa Mradi wa Ujenzi wa Bomba la mafuta ghafi
Serikali
imewasilisha Mkataba wa Kimataifa wa Mradi wa ujenzi wa bomba la mafuta
ghafi la Afrika Mashariki kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Uganga.
Akiwasilisha
Mkataba huo kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison
Mwakyembe amesema kuwa Tanzania na Uganda ni wanachama wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki ambayo malengo yake ni pamoja na kuimarisha ushirikiano
kati ya nchi wanachama kwenye maeneo ya kisiasa, kiuchumi, kijamii
kiteknolojia , utafiti, ulinzi na masuala ya Kisheria.
Dkt.
mwakyembe amesema kuwa Serikali ya Uganda kupitia kampuni za Kimataifa
za TOTAL, TULLOW NA CNOOC iligundua uwepo wa mafuta ghafi takribani
mapipa bilioni 6.5 katika eneo la Albertine nchini Uganda.
”
Kufuatia ugunduzi huo, Serikali ya Uganda ilianza kutafuta njia ya
kusafirisha mafuta hayo kwenda kwenye soko la kimataifa ambapo
iliaanisha njia takribani tatu ikiwemo ile ya kutoka Hoima nchini Uganda
hadi bandari ya Tanga nchini Tanzania” amesema Dkt. mwakyembe.
Aidha
Dkt. mwakyembe amebainisha baadhi ya faida zitokanazo na Mkataba huo
ikiwemo kuongezeka kwa mapato ya Serikali kutokana na Kodi ya zuio na
Kodi ya Mapato ya Kampuni zitakazotozwa wakati wa ujenzi na uendeshaji
wa Mradi.
Vilevile
amesema kuwa Serikali ya Tanzania itanufaika katika kuongezeka kwa
mapato ya Serikali kwa takribani Dola za Marekani 12.2 kwa kila pipa la
mafuta ghafi litakalosafirishwa kupitia Bandari ya Tanga kulingana na
kiwango cha Hisa za Serikali ya Tanzania.
”
kuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia, ulinzi na usalama kati ya
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Uganda pamoja na nchi za
Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa ujumla sambamba na kuimarika kwa huduma
mbalimbali katika bandari ya Tanga kutokana na shughuli za Mradi na
miundombinu itakayojengwa” aliongeza Dkt. Mwakyembe
Pia
ongezo kwa fursa za ajira kwa Watanzania ambapo takribani watanzania
10, 000 wataajiriwa wakati wa ujenzi na ajira zipatazo 1,000 wakati wa
uendeshaji, Amesema Dkt. Mwakyembe.
Kwa
upande wake Deogratius Ngalawa akimuwakilisha Mwenyekiti wa Kamati ya
Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ameishauri Serikali kuhakikisha
inasimamia utekelezaji wa mkataba huo kwa kuzingatia mustakabali wa
manufaa ya kiuchumi kwa Taifa.
”
Napenda kutoa pongezi za dhati kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa juhudi zake na umahiri aliouonesha
katika kuhakikisha Tanzania inapata fursa ya mradi huu mkubwa wa ujenzi
wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi kutoka Hoima, Uganda hadi Tanga,
Tanzania” Amesema Ngalawa.
Akiongea
kwa niaba ya Msemaji Mkuu kambi Rasmi ya Upinzani Wizara ya Nishati na
Madini Mhe. Devota Minja amesema kuwa bomba hilo la kusafirisha mafuta
ilikuwa na kazi iliyohusu zaidi ushawishi mpana kwani kulikuwa na
ushindani mkubwa utoka kwa nchi jirani.