SERIKALI YAWAKOMALIA MAKAHABA TANZANIA
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia Wazee na Watoto kwa ushirikiana na Wizara ya Mambo ya ndani, na
Ofisi ya rais TAMISEMI imesema itahikikisha Wanawake wanaojihusisha na
biashara ya ukahaba wanaendelea kukamatwa ili kulinda hadhi ya mwanamke.
Hayo yamebainishwa jana Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Afya
Maendeleo ya jamii, jinsia Wazee na watoto, Dkt. Hamis Kigwangala na
kuwataka kuacha mara moja na kutafuta shughuli nyingine ya kujiingizia
kipato.
Dkt. Kingwangala ametumia furasa hiyo pia kuwaasa wanaume ambao ndio
wateja wakubwa wa biashara hiyo kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo
ni kosa kisheria.
Katika hatua nyingine Dkt. Kingwangala amesema serikali imepiga hatua ya
kupambana na watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja na hatua
kadhaa wamezichukua ikiwemo kuzifungia baadhi ya taasisi zilizokuwa
zinaashiria kuwasaidia watu wa aina hiyo.