KIJANA AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUOLEWA NA MWANAUME MWENZAKE HUKO MTWARA
Mkazi mmoja wa Manispaa ya Mtwara
Sharifu Issah maarufu kamaZamda Salumu amefikishwa mahakamani kwa kosa
la kufanya vitendo vya utovu wa kimaadili kwa kujifanya mwanamke na
kumshawishi mwanaume mwenzake kufunga ndoa na kuishi pamoja kama mke na
mume.
Akisoma kesi hiyo hakimu mkuu mkazi Richard Kabate amesema kosa hilo ni
kinyume na kifungu cha 157 cha kanuni ya adhabu sura namba 16 ya sheria
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002.
Kabate amedai kuwa mshtakiwa kati ya mwezi Machi mwaka huu na mwezi wa
Juni akiwa katika vijiji vya Mkahala na Mpanyani halmashauri ya
Nanyambamkoa wa Mtwara kwa makusudi alijifanya mwanamke na kumshawishi
Mustapha Saidi Nurdini kwa kumtongoza na kufunga nae ndoa isiyo halali.
Hata hivyo hakimu Kabete amesema kitendo hicho kinatoa tafsiri ya
ukiukwaji mkubwa wa maadili kwa watu wa jinsia moja ya kiume kuishi
kinyumba.
Mshtakiwa aliposomewa shtaka hilo na wakili wa serikali George Makasi
amekana shitaka hilo na upelelezi wa kesi hiyo unaendelea mshtakiwa
amerudishw