GROUP LA WHATSAPP LA AFYA YANGU LATOA MSAADA KWA WAJAWAZITO KIBAHA MKOANI PWANI
Msimamizi Mkuu wa
Kundi la WhatsAPP la AFYA YANGU, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa
Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale (kushoto),
akimkabidhi Mbunge
wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa, vifaa vya kujifungulia wajawazito
vilivyotolewa na kundi hilo kwa Kituo cha Afya cha Mlandizi jana. Kulia
ni Mwanachama wa kundi hilo, Mudeme Elly.
Msimamizi
Mkuu wa kundi hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa
Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale (katikati), akitoa maelezo wakati
akikabidhi msaada huo.
Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya cha Mlandizi, Sahib Katyene, akitoa maelezo wakati akipokea msaada huo.
Diwani wa Mlandizi, Euphrasia Kadala, akitoa shukurani
baada ya kupokea msaada huo.
Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa, akizungumza wakati akipokea msaada huo.
Wauguzi wa kituo hicho cha afya wakipiga makofi wakati wakipokea msaada huo.
Vifaa hivyo vikipokelewa.
Mbunge wa Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa, akimkabidhi vifaa hivyo Mganga wa Kituo hicho.
Wauguzi wakipokea vifaa hivyo.
Baadhi ya majengo ya kituo hicho cha afya.
Picha ya pamoja.
Vifaa vikipelekwa kuhifadhiwa.
Ni furaha tupu baada ya kupokea msaada huo.
Waandishi wa habari wakibadilishana mawazo na Msimamizi Mkuu wa kundi hilo, ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani Lulale.
Na Dotto Mwaibale, Kibaha
KUNDI la WathAssp la Afya yangu limetoa
msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi 900,000 kwa ajili
ya kujifungulia wajawazito kwa Kituo cha Afya cha Mlandizi mkoani Pwani.
Vifaa hivyo vilivyopokelewa na Mbunge wa
Kibaha Vijijini, Humoud Jumaa vilikabidhiwa katika kituo hicho huku
tukio hilo likishuhudiwa na Diwani wa Mlandizi, Euphrasia Kadala na
wauguzi wa hospitali hiyo.
Akizungumza wakati akipokea vifaa hivyo
Mbunge Jumaa alisema msaada huo umefika kwa wakati muafaka na utasaidia
wajawazito katika hospitali hiyo.
"Msaada huu tulioupokea leo hii
utawasaidia wajawazito wanaofika kujifungua katika kituo hiki tuna
washukuru sana" alisema Jumaa.
Alisema yeye yupo katika makundi ya
WathAssap 36 lakini hajawahi kuona yakitoa msaada kwa jamii kama
lililofanya kundi hilo la AFYA YANGU ambapo alitoa ushauri kwa makundi
mengine kuiga mfano huo.
Msimamizi Mkuu wa kundi hilo, ambaye pia
ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa Kijamii wa Habarika 24, Shabani
Lulale alisema kama kundi waliguswa na kusukumwa kusaidia katika eneo
hilo kufuatia mafunzo ya afya wanayopata kutoka kwa wataalamu wa afya
ambao ni wanachama katika kundi hilo.
"Katika kundi letu tuna madaktari ambao
hutupa mafunzo kuhusu masuala mbalimbali ya afya ambapo kupitia mafunzo
hayo tukasukumwa kuchangishana na kusaidiwa na wadau wengine na kuona
tufanye hiki tulichokifanya" alisema Lulale.
Lulale alisema waliona ni vizuri msaada
huo kuupeleka nje ya mkoa wa Dar es Salaam ambako wanaamini kunachangoto
kubwa ya vifaa hivyo vya kujifungulia kwa wajawazito.
Mganga Mfawidhi wa Kituo hicho cha Afya
cha Mlandizi, Sahib Katyene alishukuru kupata msaada huo kutoka katika
Group hilo la WhatAssap na kutaka wadau wengine kuiga mfano huo.
Katyene alisema katika kituo hicho cha
afya wajawazito 250 hujifungua kwa siku kwa njia ya kawaida huku
wanaofanyiwa upasuaji wakiwa kati ya 20 na 25.
Alisema kutokana na hali hiyo licha ya
serikali kutoa bure vifaa vya kujifungulia vifaa walivyokabidhiwa na
kundi hilo vitasaidia kwa wajawazito wanaofika kujifungua katika kituo
hicho.
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)
(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712727062)