Tundu Lissu Akamatwa na Jeshi la Polisi Akiwa Kisutu
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amekamatwa leo Jumatatu mchana akitokea Mahakama ya Kisutu.
Mwanasheria
huyo alikuwa na kesi ya tuhuma za uchochezi lakini pia alikuwa ni
wakili kwenye kesi inayomkabili mfanyabiashara Yericko Nyerere
mahakamani hapo.
Akielezea
ilivyokuwa Ofisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema wakati gari
la Lissu likiwa liko getini tayari kwa kutoka, likazuiwa na nyuma ya
gari yake pia likasimama gari jingine likiwa na askari polisi wenye
silaha, kisha wengine wakamfuata na kumwambia yuko chini ya ulinzi na
atakiwa kwenda Central Police.
Baada ya hapo, wakamtaka ashuke kwenye gari lake na apande gari jingine la kwao kwa ajili ya kuelekea Central Polisi.
Tundu Lissu amekamatwa leo tarehe 22 Agosti 2017 zikiwa zimepita siku tatu toka alipotoa taarifa ya ndege ya Tanzania 'Bombadier Dash Q400' kuzuiliwa nchini Canada kutokana na amri ya mahakama
Tundu Lissu amekamatwa leo tarehe 22 Agosti 2017 zikiwa zimepita siku tatu toka alipotoa taarifa ya ndege ya Tanzania 'Bombadier Dash Q400' kuzuiliwa nchini Canada kutokana na amri ya mahakama