Makubwa Haya: MWANAMKE ALIVAA SHELA ATINGA MTAANI NA BANGO AKITAKA MWANAUME WA KUMUOA
Mwanamke mmoja nchini Kenya ameingia
katika barabara za mji mkuu Nairobi, akiwa na bango lenye maandishi
yanayosema kuwa anatafuta mwanamume wa kumuoa.
Akiwa amevaa nguo nyeupe sawa nguo inayovaliwa Bi harusi, Pris Nyambura
mwenye umri wa miaka 28, ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, alikuwa na
bango lililosema.
"Ninahitaji bwana, nina mtoto msichana wa umri wa miaka saba"