Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amezungumzia suala la
kuokotwa miili ya watu kwenye viroba katika fukwe za bahari ya Hindi, na
kusema suala hilo tayari lipo mikononi mwa Jeshi la Polisi kwa
uchunguzi zaidi.
Sirro amesema kweli taarifa hizo zimelifikia Jeshi la Polisi, na kwamba
tayari miili ipo wenye utambuzi kwa kuchukua vinasaba ili kujua ni raia
wa nchi gani, na kisha litatangaza kwa watu walipotelewa na ndugu zao
kwenda kuangalia kama ni wao.
Kamanda Siro aliendelea kwa kusema kuwa pamoja na kwamba watu
wanafikiria mauaji hayo yamefanywa na Jeshi la Polisi, wafahamu kwamba
wao kama Jeshi la Polisi huwa hawana kificho, kama wamekutana kwenye
mapambano wamewaua watu wataweka wazi kuwa wameua, na siyo kwenda
kuwatumbukiza baharini.