Kizimbani kwa kula nyama za binadamu
Watu wanne wamefikishwa mahakamani nchini Afrika Kusini kujibu mashtaka ya kula nyama ya binadamu.
Aidha, watu hao wanakabiliwa pia na mashitaka ya kupanga mauaji.
Watu hao walibainika baada ya mmoja wao kujipeleka katika kituo cha polisi na kusema kuwa amechoka kula nyama ya binadamu.
Alipohojiwa
zaidi mtuhumiwa huyo alionyesha sehemu ya mguu na mkono wa binadamu
ambavyo vilisalia baada ya kula sehemu nyingine za mwili.
Kisha
polisi wakaandamana na mtuhumiwa huyo mpaka kwenye nyumba moja
iliyopo katika mji wa KwaZulu-Natal na kushuhudia miili mingine ya
watu.
Kati ya watu hao wanne, wawili ni waganga wa jadi..