WASTAAFU PSPF MWAKA 2017/18 "KULAMBA" SHILINGI TRILIONI 1.3 ZA MAFAO

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu,
aliongozana na Mkurugenzi wa Uendeshaji Bi. Neema Muro na Mkurugenzi wa
Mipango na Uwekezaji Bw. Gabriel Silayo, baada ya kufungwa kwa semina
kwa wastaafu watarajiwa wa wilaya zote za mkoa wa Mwanza iliyofanyika
ukumbi wa chuo cha watumishi wa Benki Kuu ya Tanzania, huko Capri-point
jijini Mwanza.
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
Katika hotuba yake aliyotoa wakati wa ufunguzi rasmi wa semina hiyo, Bw.
Mayingu alisema, PSPF inatarajia kulipa wastaafu kiasi cha shilingi
Trilioni 1.3 kwa mwaka huu tu wa 2017/18."Kwa mwaka 2017/18 pekee,
Mfuko unatarajia kuwalipa wastaafu 9,552 jumla ya mafao yanayofikia
shilinginTrilioni 1.3.Kisai hiki cha Mafao ni kikubwa, hivyo kupitia
semina hii Wastaafu watarajiwa wa PSPF wamejifunza namna ya kupanga
maisha yao baada ya kustaafu ikiwa ni pamoja na fursa za uwekezaji wa
mafao yao ili mafao haya yaweze kutoa mchango mkubwa katika maendeleo
ya uchumi na kuongeza fursa za ajira." Alisema Bw. Mayingu katika
hotuba
yake.
Miongoni mwa mambo waliyojifunza wastaafu hao wanaokadiriwa kufika 450,
ni pamoja na uanzishwaji wa viwanda vidogo vidogo, namna bora ya
utunzaji fedha kwenye taasisi za fedha, (mabenki), lakini pia mbinu
mbalimbali za ujasiriamali.
Kuhsu mafunzo yaliyotolewa na SIDO, Bw. Mayingu alisema Mfuko ulikutana
na Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo (SIDO) na kujadiliana
namna ambavyo taasisi hizi mbili zinaweza kushirikiana na kuwafanya
wastaafu wa PSPF wapate ujuzi wa kuwekeza na kuweza kutengeneza ajira
kwa vijana.
"Lengo likiwa SIDO iwajengee uwezo kitaalamu na kuwapatia vifaa ili
wastaafu wa PSPF waweze kuanzisha viwanda vidogo vidogo na shughuli
nyingine za uzalishaji",lisema Bw. Mayingu.
Alisema wameamua kufanya hivyo kwa kzuingatia ukweli kuwa, katika
kufuatilia wastaafu wa Mfuko wamegundua kuwa baadhi yao hujiingiza
katika biashara mbalimbali ambazo hawakujiandaa vema na matokeo yake
kupoteza mafao yao.
Washiriki wakijadiliana
Mkurugenzi wa Masoko wa wa Mfuko wa uwekezaji wa pamoja UTT-AMIS, Daudi
Mbaga, akitoa mada ya namna wanachama wa taasisi hiyo wanavyoweza
kufaidika kwa kuwekeza kwenye Mfuko huo.
Mshiriki akizungumza kwenye semina hiyo wakati wa ufungaji wa mafunzo ya siku mbili
Mmoja wa wastaafu wa PSPF, ambaye kwa sasa ni mteja wa benki ya NMB,
akitoa ushuhuda jinsi alivyofaidika baada ya kuitumia benki hiyo pale
alipostaafu ambapo sasa anaedesha miradi mbalimbali kufuatia mikopo
anayompewa na benki hiyo na kumfanya aishi maisha ya amani.
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), Mkurugezni wa
Uendeshaji, Bi.Neema Muro, (katikati) na Mkurugenzi wa Mipango na
Uwekezaji, Bw. Gabriel Silayo, wakifurahia michango ya mawazo kutoka kwa
washiriki wa semina.
Meneja wa Mfunzo kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda vidogo vidogo SIDO,
Bi. Beata Minga, (kulia), akiongoza kikao wakati wa kufungwa kwa semina
ya siku mbili ya mafunzo kwa wastaafu watarajiwa
Mshiriki akichangia mawazo yake kwenye semina hiyo
Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (katkati), akiwa na viongozi
wengine wa Mfuko kutoka kushoto ni Meneja Mipango na Utafiti,
Bw.Luseshelo Njeje, Mkurugenzi wa Uendeshaji, Bi. Neema Muro, Mkurugenzi
wa Mipango na Uwekezaji, Bw. Gabriel Sulayo, na Meneja wa Pensehini za
Wastaafu, Bw.Mohammed Salim.
Bw. Mayingu, (kushoto), akijadiliana jambo na
Bwana Dominic Haule, Mkurugenzi IMADS, (wa kwanza kulia), wengine
wanaosikiliza kutoka kushoto ni Bi. Neema Muro, Bw. Gabriel Silayo,
Bw.Bw.Luseshelo Njeje na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul
Njaidi, baada ya kufungwa kwa semina hiyo
Mgeni Rasmi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.
Samia Suluhu Hassan, ambaye awali aliifungua rasmis semina hiyo, akiwa
katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu
Kijaji, (watatu kulia waliokaa), Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Bw.John
Mongella, (watatu kushoto), Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw. Adam Mayingu,
(wapili kulia), na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF,
Bw.Nyakimuro Muhoji, viongozi wengine na wafanyakazi wa PSPF
Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa PSPF, Bw.Nyakimuro Muhoji,
(kushoto) na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa PSPF, Bi. Neema Muro wakiwasili
ukumbini
Naibu waziri wa fedha na mipango, Dkt. Asshatu Kijaji, Kaimu Mwenyekiti
wa Bodi ya Wadhamini ya PSPF, Bw. Nyakimuro Muhoji (katikati) na
Mkurugenzi Mkuu, Bw. dam Mayingu wakiwasili ukumbini.