HATIMAYE ZITTO KABWE AFUNGUKA KUHUSU ANNA MGHWIRA KUTEULIWA NA RAIS MAGUFULI KUWA MKUU WA MKOA WA KILIMANJARO
Zitto Kabwe
Rais Dk. John Magufuli jana amemteua Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam na
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais-Ikulu, Gerson Msigwa, mwenyekiti huyo
wa chama cha upinzani, anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Said Meck
Sadiki.
Baada ya kukaa kimya kufuatia uteuzi huo hatimayeLeo Jumapili June
4,2017 Kiongozi wa AICT Wazalendo Zitto Kabwe ametoa ujumbe yafuatayo:
"Nimekuwa naulizwa Sana kuhusu uteuzi wa Mwenyekiti wa Chama chetu
kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro. Nimekuwa kimya Kwa sababu tumepokea
Taarifa za uteuzi kutoka katika vyombo vya Habari. Mwenyekiti yuko nje
ya nchi na kutokana na tofauti za masaa bado hatujawasiliana nae.
Tutatoa tamko kamili atakapokuwa amerejea nchini.
Ninawataka wanachama wote wa Act Wazalendo wawe watulivu na Kama kuna
masuala yanayohusu maamuzi ya vikao vya Chama tutawajulisha.
Kabwe Zuberi Ruyagwa Zitto,Mb
Kiongozi wa Chama"