WADAU WA PSPF WAWATANGAZIA FURSA WASTAAFU WATARAJIWA
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Mwanza
MFUKO wa Pensheni wa PSPF umewaleta poamoja watumishi wa umma kutoka
wilaya zote za mkoa wa Mwanza zaidi ya 450, ambao wanatarajiwa kustaafu
hivi karibuni ili kuwapatia semina ya mafunzo itakayowawezwesha
kujiandaa kustaafu kwa amani.
Katika semina hiyo iliyoanza leo Juni 2, 2017 kwenye ukumbi wa chuo cha
BoT Capri-point jijini Mwanza, wadau wa PSPF ambao ni taasisi za fedha
nao wametumia fursa hiyo kutangaza fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao
wanaweza kuzitumia ili kuendeleza maisha yao ya baadaye.
Wadau hao ni pamoja na Mwalimu Commercial Bank, (MCB), NMB, CRDB, TPB na
Mfuko wa UTT-AMIS, pia Shirika la Viwanda Vidogo vidogo SIDO.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara na Masoko, Mwalimu Commercial Bank,
(MCB),Bw. Valence Luteganya, akizungumzia huduma mbalimbali zitolewazo
na benki hiyo. "Beni hii imeanzishwa hivi karibuni na wamiliki wa benki
hii kwa karibu asilimia 30 ni walimu. na huduma tunazozitoa ni pamoja na
utoaji mikopo nafuu, ushauri wa kifedha lakini pia katika jiyihada za
kurahisisha huduma za kibenki, MCB imo kwenye mtandao wa Umoja Switch
ambao umetapakaa nchi nzima." hayo ni baadhi ya maneno ya Bw.
Lutenganya
Bw. Lutenganya, akifafanua zaidi huduma zitolewazo na benki ya MCB
Mkuu wa kitengo cha wateja binafsi benki ya NMB, Bw.Omary Mtiga, akitoa
somo kuhusu fursa mbalimbali ambazo wastaafu hao watarajiwa wanaweza
kuzipata. "Benki ya NMB ina matawi kote nchini na hivyo inaweza
kukufikishia huduma
hapo ulipo pasina shaka, kwenu nyinyi ambao wengi wenu ni wateja wetu,
mnayo fursa ya kufungua Bonas account ambayo inakuwezesha kufikia
malengo mbalimbali uliyojiwekea na inaweza kutunza amana zako kwa
usalama na kufikia malengo yako ya baadaye uliyojiwekea, lakini kubwa
zaidi hakuna gharama za kuendesha akaunti
hii." alisema
Mkurugenzi wa idara ya mikopo benki ya Posta Tanzania, (TPB), Bw. Henry
Bwogi, akizoa mada kwa washiriki ambapo alisema, "TPB ndiyo benki kongwe
kuliko zote hapa nchini ikiwa na matawi yaliyosambaa kila kona ya nchi
na hivyo kuwa rahisi kwa wateja kufikiwa na huduma zake, lakini pia
benki hiyo tayari imeonyesha nia ya dhati ya kuwajali wastaaafu ambapo
imekwisha toa mikopo ya mabilioni ya shilingi kwa wanachama wa Mfuko wa
Pensheni wa PSPF.
Bi Doris Mlenge, Afisa Masoko wa Mfuko wa UTT-AMIS, akiwapatia
vipeperushi vyenye maelezo ya huduma mbalimbali zitolewazo na Mfuko huo.
"Kwa mtu yeyote anayetegemea kupata kipato kwa mkupuo kutokana na
pensheni au chanzo kingine cha fedha anatakiwa kuwekeza kwenye Mfuko huo
ili aweze kupata kipato cha mara kwa mara na akasema kuwekeza kwenye
mifuko ya kujikimu kama UTT-AMIS kunatoa faida kubwa ukilinganisha na
uwekezaji wa namna hiyo kwenye masoko ya fedha.
Bw. Denis Mwoleka, ambaye ni Meneja wa CRDB tawi la Chuo Kikuu cha SAUT
jijini Mwanza, akizungumza kuhusu umuhimu wa wastaafu hao watarajiwa
kujiunga nabenki hiyo kwa kutarajia kupata faida mbalimbali ikiwemo
huduma mpya ya akaunti ya akiba ya dhahabu ambayo ni njia rahisi ya
kujiwekea akiba ili kufanikisha malengo ya baadaye.
Afisa kutoka Shirika la viwanda vidogo vidogo SIDO, akihamasisha
wastaafu watarajiwa kuwekeza kwenye uanzishaji wa viwanda vidogo vidogo
ambavyo vitawawezesha kujikimu kimaisha na ksutaafu kwa amani. yeye
alsiema SIDO iki tayari kutoa ushauri na mafunzo ya uanzishaji wa
viwanda hivyo
Meneja Pensheni za Wastaafu wa PSPF, Bw.Mohammed Salim,(kulia),
akifurahia jambo na Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa PSPF, Bw.
Gabriel Silayo, (wapili kushoto) na Meneja Mipango na Utafiti wa Mfuko
huo, Bw.Luseshele Njeje
Meneja wa Fedha wa PSPF, Bw.Lihami Masoli. (kulia), na Mtafiti
Mwandamizi wa Mfuko huo, Bw.Mapesi Maagi, (katikati), wakibadilishana
mawazo na Katibu Msaidizi wa TSC wilaya ya Kwimba, Bw. Fundikira R.K.
James, wakati wa mapumziko ya semina hiyo
Meneja Pensheni za Wastaafu wa PSPF, Bw.Mohammed Salim, (kushoto), akifafanua mambo kadhaa kuhusu pensheni
Bw. Silayo (kushoto), akiteta jambo na Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi