Home habari SERIKALI KUSAFIRISHA MWILI WA MZEE NGOSHA ALIYECHORA NEMBO YA TAIFA SERIKALI KUSAFIRISHA MWILI WA MZEE NGOSHA ALIYECHORA NEMBO YA TAIFA
Mwili wa Mzee Francis Maige Kanyasu alimaarufu kwa jina la Mzee Ngosha
ambaye anayetajwa kuwa ni moja wa wachoraji wa nembo ya Taifa
aliyefariki tarehe 30 mwezi wa 5 unatarajiwa kusafirishwa leo kuelekea
Misungwi Mwanza.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Wizara ya Afya (Maendeleo ya Jamii)
imesema kuwa ndugu wa Mzee Kanyasu wamepatikana na sasa serikali
itagharamia kusafirisha mwili wa mzee huyo mpaka Mwanza ambapo atakwenda
kuzikwa huko.
Mwili wa Mzee Francis Maige unatarajiwa kuagwa leo Jumamosi saa 2
asubuhi Hospitali Taifa ya Muhimbili kabla ya kuanza safari ya kuelekea
Mwanza.