Bodaboda Achinjwa Kinyama na Kuporwa Pikipiki
Mwanaume
mmoja (30) mkazi wa Nyankumbu wilayani Nyamagana mkoani Geita
anashikiliwa na jeshi la polisi kwa kosa la mauaji ya dereva bodaboda
yaliyotokea majira ya 3:00 Usiku tarehe 06.05.2017.
Kaimu
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza ACP Zarau Mpangule amemtaja mtuhumiwa
huyo kuwa ni Andrea anayedaiwa kupora pikipiki na kumuua dereva wa
pikipiki Bw. Alphonce Sekagi (32) mkazi wa wilayani Sengerema
wakilishirikiana na wenzake wawili kisha kutoroka na pikipiki
kusikojulikana.
Taarifa
zinaeleza kuwa marehemu alikuwa dereva bodaboda wa mji wa Sengerema na
siku ya tukio alipakia abiria watatu kwenye pikipiki yake wakitokea
Sengerema mjini kwenda kijiji cha Tabaruka na kwamba wakati wakiwa
njiani abiria hao walimkata dereva huyo na kitu chenye ncha kali
shingoni kisha wakamchinja kwa kutumia panga shingoni na kupelekea
kupoteza maisha papo hapo.
Kamanda
Mpangule amesema wananchi walitoa taarifa polisi kuhusiana na tukio
hilo ambapo askari walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na
kufanya msako mkali wa kuwatafuta watuhumiwa wa mauaji hayo katika
maeneo mbalimbali kwa kushirikiana na wananchi ndipo tarehe 01.06.2017
majira ya saa 8:30 mchana wakafanikiwa kumtamata mtuhumiwa mmoja akiwa
na pikipiki waliyoipora katika mauaji hayo.
Kamanda
Mpangule ameendelea kwa kusema upelelezi na msako wa kuwatafuta
watuhumiwa wengine wawili ambapo wanadaiwa kushiriki katika mauji hayo
pamoja na uporaji unaendelea huku mtuhumiwa aliyekamatwa anafanyiwa
mahojiano na uchunguzi ukikamilika atapandishwa mahakamani.