MWEKEZAJI AWAPATIA MAJI WANANCHI.
Mashine ya kuchimba visima virefu ikiwa inatoa maji. |
Wananchi wa kijiji cha Nduha na Mwamlapa wakiwa katika eneo la kisima cha maji. |
Diwani wa kata ya Kasoli Mayala
Nshiminzi akimwonyesha namna maji meneja wa kiwanda Boaz Ogolla yalivyopatikana
wakati wa zoezi la uchimbaji wa kisima hicho kijiji cha Mwamlapa.
Na COSTANTINE MATHIAS, Simiyu.
WANANCHI na wakazi wa vijiji vya
Mwamlapa na Nduha kata ya Kasoli wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamenufaika na
mradi wa maji wa kisima kirefu kilichochimbwa na mwekezaji wa kiwanda cha kuchambua
pamba cha Alliance Ginnery kwa lengo la kusogeza huduma hiyo kwa jamii.
Akizungumza jana wakati wa zoezi la
uchimbaji wa kisima hicho likindelea, Meneja wa kiwanda hicho Boaz Ogola
alisema kuwa kisima hicho kitaghalimu kiasi cha milioni 30 ambapo maji
watayatoa kwenye kisima na kupeleka katika kijiji hicho pamoja na kijiji cha
Ndilu.
Ogola alisema kuwa katika mradi hiyo
pamoja na mingine vitachimbwa katika kata hiyo ambapo visima vitano vitaghalimu
kiasi cha milioni 200 lengo likiwa ni kusogeza huduma za kijamii .
“katika bajeti yetu tutenga milioni
200 kwa ajili ya kuchimba visima virefu katika kata hiyo na wananchi
tumeshawashirikisha na wameitikia kwani visima hivyo vitasaidia jamii kufanya
shughuli za kimaendeleo kwa kiasi kikubwa tofauti na sasa hasa wakinamama muda
mwingi wanahangaika kuchota maji”alisema Ogola.
Alibainisha kuwa wao kama wawekezaji
watahakikisha jamii wanayoishi nayo wanaisaidia katika miradi mbalimbali ya
maendeleo kwani bila wananchi kujishughulisha hata uwepo wa kiwanda hicho ni
sawa na bure na kwamba hakiwezi kufanya shughuli ya uzalishaji.
Kwa upande wake diwani wa kata hiyo
Mayala Lucas alisema kuwa hali ya ukosefu wa maji katika kijiji hicho ulikuwa
mkubwa na kwamba walikuwa wanalazimika kufuata maji mbali na kijiji hicho.
Mayala alisema kuwa baada ya kupata
mradio huo kutoka kwa mwekezaji kijiji kilikaa na kujadiliana jinsi ya kupata
eneo la kuchimba kisima ambapo wananchi walikubali kuachia maeno ili wataalamu
wa maji wapime sehemu ambayo wanaweza kupata maji hayo.
Aidha alisema kuwa kuwepo kwa mradi
huo utanufaisha wakazi 5000 wa vijiji viwili vya Mwamlapa na Ndilu na
kuachana na changamoto ya maji ya mda mrefu katika vijiji hivyo kwani maji hayo
yatavutwa kwa umeme kuelekea katika sehemu husika ya kuchotea maji.
Alisema katika kushirikiana na
serikali Halmashauri ya wilaya ya Bariadi vijijini wanao mpango wa kuvuta maji
kutoka katika visima hivyo kusambaza katika vitongoji vyake kwani mwekezaji
atavuta kuelekea kwenye senta ambapo kutakuwa na kituo kikubwa cha kuchota
maji.
Maria John ambaye ni mkazi wa kijiji
hicho alisema kuwa kuwepo kwa mradi wa kisima hicho utawapunguzia adha ya maji
iliyokuwepo awali kwani walikuwa wakilazimika kufuata maji umbali wa kilomita 3
hadi 4.
Alibainisha kuwa endapo mradi huo
ukitunzwa kikamilifu wananchi watanuika hivyo amewataka wananchi wa kijiji
hicho kutoa ushirikiano kwa mwekezaji huyo ili aendelee kusaidia katika miradi
mingine.