PLUIJM ATAKA KUANZA KUONYESHA MAJONJO YAKE SPORTPESA SUPER CUP
Kikosi cha Singida United kitaendelea na mazoezi yake leo kujiandaa na michuano ya Sport Pesa Super Cup.
Kocha Mkuu wa Singida United, Hans van
der Pluijm, amesema michuano hiyo itakuwa ni sehemu ya kujiandaa na Ligi
Kuu Bara lakini kutengeneza morali ya kikosi chake.
“Kuna mabingwa wa ligi kuu, mabingwa wa
kombe la shirikisho. Lakini kuna timu kutoka Kenya, haitakuwa michuano
rahisi kwa timu mpya kama yetu.
“Lakini tunataka kucheza soka safi na la
ushindani na kushinda ili kujenga morali lakini kuendelea kujenga
kikosi chetui kabla ya ligi kuu ukiwa ni msimu wa kwanza,” alisema
Pluijm.
Timu nyingine za Tanzania Bara zilizo katika michuano hiyo ni Simba na Yanga wakati Jang’ombe inatokea Zanzibar.
Timu kutoka Kenya ni Gor Mahia, AFC Leopards na Nakuru All Stars.