Marekani Yaionya China
Marekani
imeionya China kuhusu mpango wake wa kupeleka wanajeshi wake katika
visiwa ilivyojenga baharini kusini mwa nchi hiyo kwaajili ya kujilinda
na maadui wa taifa hilo.
Onyo
hilo limetolewa na Waziri wa ulinzi wa Marekani, James Mattis katika
mkutano wa kujadili masuala ya usalama uliofanyika Singapore, ambapo
amesema kupeleka wanajeshi katika visiwa hivyo kutahatarisha amani ya
dunia.
Aidha,
ameongeza kuwa kama China itaendelea na mpango wake wa kupeleka
wanajeshi katika visiwa hivyo, kuha hatari kubwa uhusiano kati ya nchi
hizo kuvurugika na kuhatarisha amani ya eneo hilo.
Hata
hivyo, hatua hiyo ya Marekani imekuja mara baada ya Baraza la Usalama
kuiongezea vikwazo Korea ya Kaskazini kufuatia kufanya majaribio kadhaa
ya makombora ya masafa marefhu.