Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Nyanswi ashambuliwa Polisi w...
Watu
watatu wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za Kushambulia na
kumuumiza mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tarime mkoani Mara Hamis
Nyanswi.
Tukio
hilo lilitokea april 14 saa tatu usiku katika mtaa wa kibasa mjini hapa
wakati mwenyetiki wa halmashauri Hamis Nyanswi akitoka kwenye shughuli
zake za kawaida ndipo aliweza kukutwa na tukio hilo.
Akisimulia
mkasa huo huku akiongea kwa shida akiwa amelazwa katika kituo cha afya
cha DF Tarime, Nyanswi amesema akiwa wakati anaenda kwake aliwaona watu
watatu wakiwa barabarani na kuwagongea honi ili wapishe apite lakini
walimsimamisha na kuanza kugonga kioo cha gari lake wakiashiria afungue,
na kufanya hivyo na ndipo alianza kushambuliwa.
Ameongeza
kuwa baada ya tukio hilo alifanikiwa kunyanyuka na kuchukua bunduki yake
iliyokuwa imeanguka chini mtaroni na kufyatua risasi mbili hewani
ambapo wawili kati ya wawatu hao walifanikiwa kukimbia, huku mmoja
akianguka mtaroni na na badae Nyanswi kupiga Simu Polisi na Mtuhumiwa
huyo kukamatwa na Polisi.
Kamanda wa Polisi Tarime Rorya Henry
Mwaibabmbe akiongea na CLE24NEWS kwa njia ya Simu amesema kuwa tukio
hilo linausishwa na suala la ulevi na watuhumiwa wote wanashiliwa na
jeshi la polisi kwa ajili ya mahojiano huku akiitaka jamii kuwa suala
hilo lisiingizwe Siasa.
,,,SIKILIZA HAPA CHINI KAMANDA PAMOJA NA MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA MJI WA TARIME NYANSWI,,.