OFISA WA SERIKALI AJIFUNGUA WATOTO WANNE KWA MPIGO
Ofisa Tarafa wa Kibamba, wilayani
Ubungo, Beatrice Mbawala amejifungua watoto wanne kwa mpigo katika
Hospitali ya Agha Khan, jijini Dar es salaam.
Beatrice amejifungua watoto hao wakiwa njiti mwezi mmoja uliopita.
Akizungumza hospitalini hapo, Machi 3,
baba wa watoto hao, Julius Mbawalla amesema familia yake ina furaha
kupokea watoto wanne na kwamba jukumu lake kubwa ni kuhakikisha mkewe
anapata huduma muhimu ili aweze kumudu kuwanyonyesha.
Daktari Bingwa wa Watoto katika
hospitali ya Agha Khan, Dk Mariam Mgonja amesema afya za watoto
zimeimarika na tayari wameruhusiwa kwenda nyumbani.